Misemo ya Kiiraqw — Methali za Wairaqw (Iraqw Proverbs)

Methali na misemo ya jamii ya Wairaqw kutoka Mbulu, Manyara — maana kamili kwa Kiswahili na Kiingereza.

Kiiraqw (pia Iraqw, Wairaqw, Mbulu) ni lugha ya Kikushitiki inayozungumzwa na watu zaidi ya laki mbili katika wilaya ya Mbulu na Karatu, Mkoa wa Manyara. Misemo — methali za maisha — ni hazina ya hekima, subira, uaminifu, malezi na maadili ya jamii. Mkusanyiko huu una misemo kutoka kwa wachangiaji wa jamii na utafiti wa Shaaban & Mwangosi (Nafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw), ulioratibiwa kwa Nukta Kamusi ili kuhifadhi lugha na utamaduni.

Kiiraqw (Iraqw, Wairaqw) is a Cushitic language of northern Tanzania. Wairaqw misemo are oral proverbs passed down by elders in Mbulu society — teaching patience (subira), integrity (uaminifu), parenting (malezi), hard work, and community harmony. Each entry includes the original Kiiraqw saying, a Swahili equivalent, an English gloss, and cultural explanation.

Full Kiiraqw dictionary Salamu & phrases Kamusi PDF Swahili → Kiiraqw Kiiraqw → Swahili Changia misemo Home

Misemo Mengine

Misemo mingine ya Kiiraqw

Kiswahili: Mimi ni mkali, vitu vyangu ni vya kulipa.

I am fierce; my things must be paid for.

Soma zaidi
Unasisitiza kuwa dawa ya deni ni kulipa. Jamii ya Wairaqw inasisitiza haki na usawa; watu huishi kwa maadili waliyorithishwa kutoka vizazi tangu kale. Jamii inakataza kudhulumu amana isiyo ya halali. Mtu akikopa amana ya mwingine ni sharti alipe kabla hajachukuliwa hatua kwa mujibu wa jamii.

Kiswahili: Baba wa kukuzaa kama hayupo, hata wa malezi hayupo?

If the birth father is absent, is there even a parent for upbringing?

Soma zaidi
Unatoa picha kuwa malezi ya mtoto hayategemei kuwepo kwa wazazi wawili. Jamii nzima ina jukumu la kuhakikisha watoto wanalelewa na kujengwa katika misingi ya uzalendo, utamaduni na maadili ya jamii. Mtoto ni mali ya jamii nzima; jamii ya Wairaqw inashirikiana kuwalea watoto kwa mujibu wa utamaduni wao.

Kiswahili: Ukienda sehemu beba kibuyu cha njiani.

When you go somewhere, carry a gourd for the journey.

Soma zaidi
Inasisitiza umuhimu wa kujiwekea akiba ili kuepuka fedheha kwa kuwa matatizo hayapigi hodi. Binadamu yeyote anatakiwa kujiandaa katika maisha yake kwani safari ni hatua moja baada ya nyingine. Maisha ni safari iliyojaa adha kadha wa kadha, ambazo haziepukiki.
Jamii haina budi kuweka akiba itakayomsaidia mtu anaposafiri ili waliobaki nyumbani waendelee kuishi vizuri. Jamii inapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuweka akiba itakayosaidia kumudu harakati za maisha ya kila siku katika jamii.

Kiswahili: Ukikataa kuonywa, kitakachokukuta utakataa.

If you refuse warning, you will refuse what befalls you.

Soma zaidi
Unamaanisha watu wanapaswa kukubali ushauri wanaopewa na watu wazima katika jamii yao. Ni sawa na methali 'Mkataa pema pabaya panamwita'. Wanajamii wanakumbushwa kufuata mambo yenye tija kwa manufaa ya familia na jamii zao.

Kiswahili: Hasira za mtawala ni kama ngurumo ya simba.

A ruler's anger is like a lion's roar.

Soma zaidi
Unasisitiza kuwa kiongozi anayechaguliwa anaweza kufanya jambo lolote kulingana na mamlaka aliyonayo, lakini lazima atende haki kwa vitendo kwani anachokisema kisikilizwe na kufanyiwa kazi. Msemo huu unasisitiza namna ya kuwaheshimu viongozi katika mambo yenye tija katika jamii.

Kiswahili: Muda wa masika ni mbili.

The rainy season is short.

Soma zaidi
Ukichelewa kulima na kupanda mapema hautapata mavuno ya kutosha kwa wakati. Kushindwa kumudu mahitaji ya wakati, watoto watapata njaa hali waliowahi kulima watapata mazao ya kutosha. Jamii inashauriwa kuzingatia muda na kulima kwa kufuata kanuni za kilimo na ufugaji ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa misimu husika.

Kiswahili: Nyumba ni sawa na ng'ombe mwenye mguu mbovu.

A house is like a cow with a lame leg.

Soma zaidi
Inamaanisha umuhimu wa kuwa na subira katika jamii. Wazazi wanapaswa kuishi kwa subira kwani wanandoa wanapokutana na kuishi pamoja kila mmoja na tabia zake zinazoweza kusababisha kuhitilafiana. Uamuzi wa busara unatakiwa kabla ya kulifanyia kazi jambo lolote.

Kiswahili: Uwindaji wa vijana, tai huwafuata.

When youths hunt, the eagle follows them.

Soma zaidi
Humaanisha kuwa vijana wana uwezo wa kufanya jambo lolote zuri au baya. Busara za wazazi huwapa fursa pana ya kufuatilia kile walichokiona kibaya na kuomba msamaha kwa yeyote aliyetendewa.
Jamii ya Wairaqw inaamini kuwa kutenda haki kunaepusha laana, visasi na mafarakano. Katika msemo huo, wazee wanafananishwa na tai kwa kuwa anaheshimiwa sana katika jamii hiyo. Wazazi hawana budi kuwaongoza vijana kwa ustawi na uendelevu wa jamii na kizazi chao.

Kiswahili: Ndugu.

sibling / brother or sister

Kiswahili: Ndugu wapendane wawe pamoja na wazae pamoja.

Siblings should love one another, stay together and bear children together.

Soma zaidi
Msisitizo ni suala la upendo ili kujenga umoja na mshikamano katika jamii. Jamii ya Wairaqw inasisitiza ndugu na jamii nzima kupendana na kushirikiana ili kuondoa hali ya kuhitilafiana isiyo na tija kwa ustawi na uendelevu wa jamii.

Kiswahili: Mwewe mwenye mimba utamtambua juu.

The pregnant eagle will recognize it from above.

Soma zaidi
Inasisitiza kuwa baadhi ya maneno hayatamkwi hadharani bali hutumia lugha ya uficho ili kulinda staha za jamii inayohusika. Hali hiyo huisaidia jamii kutenda haki na kutumia busara katika kusuluhisha masuala fulani fulani katika jamii.
Jamii hiyo hutumia wazee na wanajamii kwa jumla ili kufanya suluhu katika jamii kwa busara ya hali ya juu bila ubaguzi wa aina yoyote.

Kiswahili: Mguu wa mbu utupelee.

The foot of a mosquito lifts us.

Soma zaidi
Inamaanisha kuwa binadamu wanapaswa kupendana na kusaidiana katika hali ya raha na tabu. Kwa mfano, jirani akitembelewa anakula hata kama ni kidogo.
Msemo huo una maana kuwa licha ya kuwa kilichopo ni kidogo, lazima wagawane kama sehemu ya kusaidiana.

Kiswahili: Nyumba za wapenda kesi wengi zinapotea.

Houses of those who love disputes perish.

Soma zaidi
Unatoa dhamira kuwa jamii na watu waliozoea kesi muda wowote maisha yao yanaweza kuharibika kutokana na kutokuwa na uaminifu na kuingilia mambo yasiyowahusu. Mtu aliyezoea kuhalalisha ubatili mwisho wake maisha yake huharibika pamoja na familia kukosa mwelekeo. Jamii haina budi kutenda haki ili kuepusha laana, lawama, chuki, visasi na mafarakano.

Kiswahili: Asubuhi ni kiraka.

Morning is a sieve (time is short).

Soma zaidi
Unamaanisha shughuli yeyote ya msingi ni vizuri ifanyike asubuhi ili kuifanya kwa ufanisi. Mchana kuna hali ya kuchoka kutokana na jua kali. Ni vizuri kuwajibika asubuhi ili kuendelea kumudu changamoto zinazoweza kutokea baadaye. Unafanana na 'Asubuhi kazi, jioni mahesabu'.

Kiswahili: Mdudu wa mahindi atafika tu kwake.

The maize pest will only reach him.

Soma zaidi
Mdudu huyo hutembea polepole, lakini atafika tu anakokwenda. Jambo lolote hata kama lina ugumu kupita kiasi, ipo siku litafanikiwa, hasa kama litawekewa misingi imara inayoonesha namna bora ya kulitekeleza kwa nadharia na vitendo (Darco, 2006). Kwa hakika, 'Mwenda pole hajikwai', na 'Mvumilivu hula mbivu'.

Kiswahili: Ukiwatuma watoto shambani, nao watawatuma watoto wenzao.

If you send children to the farm alone, they will send each other away.

Soma zaidi
Una maana kuwa ukiwatuma watu wakafanye kazi bila kusimamiwa huzembea na kuharibika kinachofanyika. Wazazi wanapaswa kuwajibika na kusimamia shughuli yoyote ili kuepuka jambo lisiharibike. Wazazi wana jukumu la kuwafundisha kazi watoto wao na kuhakikisha wamefanya vizuri kwa kuwafuatilia na kuwarekebisha kimaadili.

Kiswahili: Kichaka kinasikia.

The bush hears.

Soma zaidi
Unalenga kuishauri jamii kujenga uaminifu ili kuepuka migogoro isiyo na tija. Jamii inapaswa kusema ukweli ili kumweka kila mmoja huru. Hakuna siri ya watu wengi; kumsema, hasa kumsengenya mtu, kunaweza kusababisha kutoelewana. Uaminifu huwafanya watu kuishi huru na kutokuwa na wasiwasi.

Kiswahili: Ndege mwoga ana watoto wengi.

A timid bird has many chicks.

Soma zaidi
Unaifunza jamii kuepuka mambo yanayoweza kuyagharimu maisha. Jamii ya Wairaqw inachukulia kuwa mtu mwoga si mwepesi kutenda kinyume na kaida zilizopo. Mtu mwaminifu mara nyingi hutekeleza jambo lililokubaliwa na jamii kwa kufuata mipaka ya makubaliano. Msemo huu huonesha umuhimu wa uaminifu kama nyenzo ya kuishi kwa amani na utulivu.

Kiswahili: Maeneo ya watu yabebwe kwa pamoja.

People's places should be borne together.

Soma zaidi
Inamaanisha kuwa watu wasiharibu vitu vya watu na wala mtu asisemwe ubaya kwani yote hayo huharibu upendo na kusababisha hali ya uvunjifu wa amani katika jamii. Jambo la msingi ni kuwafahamu watu na tabia zao ili kuweza kuishi kwa upendo bila kufarakana.

Maswali Yanayoulizwa Sana — Kiiraqw Proverbs FAQ

Methali za Kiiraqw ni nini?

Methali za Kiiraqw (misemo ya Wairaqw) ni semi za jadi zinazofundisha maadili, subira, uaminifu na maisha ya jamii. Kila msemo una maandishi ya Kiiraqw pamoja na tafsiri ya Kiswahili na Kiingereza.

What are Kiiraqw proverbs called?

In the Wairaqw (Iraqw) community they are known as misemo — traditional sayings that teach wisdom, patience, integrity, parenting, and community values. On Nukta Kamusi we document them with Kiiraqw text plus Swahili and English translations.

Je, Kiiraqw na Iraqw ni lugha moja?

Ndiyo. Kiiraqw, Iraqw na Wairaqw ni majina ya lugha ile ile inayozungumzwa Mbulu na Karatu, Manyara. Majina mengine ni Asa na Iraku.

Is Kiiraqw the same as Iraqw?

Yes. Kiiraqw, Iraqw, and Wairaqw refer to the same Cushitic language spoken in Mbulu and surrounding areas of northern Tanzania. Alternate names include Asa and Iraku.

What does the Kiiraqw proverb "Nanagi doos gu ghoer" mean?

In Swahili: "Mdudu wa mahindi atafika tu kwake." In English: "The maize pest will only reach him." It teaches patience and perseverance — slow, steady effort eventually succeeds.

"Kichaka kinasikia" maana yake nini kwa Kiiraqw?

Hii ni methali ya Kiswahili inayolingana na msemo wa Wairaqw unaosisitiza uaminifu na ukweli — siri hazifichiki; kusema ukweli huleta amani na huruma katika jamii.

Where do Kiiraqw proverbs come from?

Many entries on this page come from Shaaban & Mwangosi's study Nafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw (Mbulu), plus community contributors on Nukta Kamusi. Misemo are used by elders to teach youth in Wairaqw society.

Where is Kiiraqw spoken?

Kiiraqw is spoken mainly in Mbulu District and Karatu, Manyara Region, Tanzania, by the Wairaqw people. It belongs to the Cushitic branch of Afro-Asiatic languages.

How many Kiiraqw proverbs are in this collection?

This page lists 57 Wairaqw misemo with Swahili and English meanings, from community contributors and the Shaaban & Mwangosi study in Mbulu.

Ni methali ngapi za Kiiraqw ziko hapa?

Ukurasa huu una misemo 57 ya Wairaqw (Kiiraqw/Iraqw) pamoja na maana za Kiswahili na Kiingereza.

What is the Swahili meaning of "Anu"?

The Kiiraqw proverb "Anu" means: "Mimi.". English: "I".

What is the Swahili meaning of "Anu lach murue a buut"?

The Kiiraqw proverb "Anu lach murue a buut" means: "Mimi ni mkali, vitu vyangu ni vya kulipa.". English: "I am fierce; my things must be paid for.".

What is the Swahili meaning of "Baba"?

The Kiiraqw proverb "Baba" means: "Baba.". English: "father".

What is the Swahili meaning of "Baba o xwayla bir kahh o haraaye ikahi?"?

The Kiiraqw proverb "Baba o xwayla bir kahh o haraaye ikahi?" means: "Baba wa kukuzaa kama hayupo, hata wa malezi hayupo?". English: "If the birth father is absent, is there even a parent for upbringing?".

Chanzo: Shaaban & Mwangosi, Nafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw (Mbulu), pamoja na michango ya jamii. Unaweza kuchangia misemo zaidi kupitia Unasemaje.