Msemo / MethaliNanagi doos gu ghoerMdudu wa mahindi atafika tu kwake.The maize pest will only reach him.
Nanagi doos gu ghoer
phrase
proverb | theme: subira, uvumilivu
swh: Mdudu wa mahindi atafika tu kwake.
en: The maize pest will only reach him.
source: Shaaban & Mwangosi — Nafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw
Soma zaidi
Mdudu huyo hutembea polepole, lakini atafika tu anakokwenda. Jambo lolote hata kama lina ugumu kupita kiasi, ipo siku litafanikiwa, hasa kama litawekewa misingi imara inayoonesha namna bora ya kulitekeleza kwa nadharia na vitendo (Darco, 2006). Kwa hakika, 'Mwenda pole hajikwai', na 'Mvumilivu hula mbivu'.
proverbscultureagriculturecontributor-seedproverbshaaban-mwangosi