How do you say "Ukienda sehemu beba kibuyu cha njiani." in Kiiraqw?Unasemaje "Ukienda sehemu beba kibuyu cha njiani." kwa Kiiraqw?
Bara amoker ghumta lohi huek
phrase
proverb | theme: akiba, maandalizi
swh: Ukienda sehemu beba kibuyu cha njiani.
en: When you go somewhere, carry a gourd for the journey.
source: Shaaban & Mwangosi — Nafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw
Soma zaidi
Inasisitiza umuhimu wa kujiwekea akiba ili kuepuka fedheha kwa kuwa matatizo hayapigi hodi. Binadamu yeyote anatakiwa kujiandaa katika maisha yake kwani safari ni hatua moja baada ya nyingine. Maisha ni safari iliyojaa adha kadha wa kadha, ambazo haziepukiki.
Jamii haina budi kuweka akiba itakayomsaidia mtu anaposafiri ili waliobaki nyumbani waendelee kuishi vizuri. Jamii inapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuweka akiba itakayosaidia kumudu harakati za maisha ya kila siku katika jamii.
proverbscultureeconomycontributor-seedproverbshaaban-mwangosi