Cha kuazima hakina manufaa ya kudumu. Jamii haina budi kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uwezo wa kumiliki mali yake. Kitu cha kuazima kitachukuliwa pindi mwenye nacho atakapokihitaji. Ni sawa na nguo ya kuazima haisitiri matako. Uvivu ni utumwa unaoondoa uwezo wa kujiamini.