Ak'vambaga makono atabulagagwa
Kiswahili: Aombaye msamaha hauawi.
One who asks for forgiveness is not killed.
Misemo ya Kisukuma yenye tafsiri ya Kiswahili na Kiingereza — hekima ya jamii ya Wasukuma.
Kisukuma ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa na Wasukuma katika Mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na maeneo jirani. Methali (misemo) ni hazina ya hekima kuhusu kazi, umoja, malezi, uaminifu na maisha ya kila siku. Mkusanyiko huu unaleta methali za Kisukuma pamoja na maana zake kwa Kiswahili.
Kisukuma is a Bantu language of the Sukuma people in northwestern Tanzania. These methali (proverbs) teach work ethic, unity, parenting, honesty, and everyday wisdom. Each entry includes the Kisukuma saying with Swahili and English meanings.
Misemo mingine ya Kisukuma
Ak'vambaga makono atabulagagwa
Kiswahili: Aombaye msamaha hauawi.
One who asks for forgiveness is not killed.
Akalemela mbasa sumvua na nyabahanda
Kiswahili: Shoka limeshindwa kukata sembuse mundu?
If the axe failed to cut, what about a blunt knife?
Kiswahili: Miguu yangu inukeni tukale vya wakulima, mvivu huishi kwa jasho la wenziwe.
My feet, rise so we may eat the farmers' food — the lazy live off others' sweat.
Kiswahili: Chakula kilichomo tumboni huwezi ukamgawia mwenzio hata kama anakufa.
Food already in the stomach cannot be shared with a companion, even if they are dying.
Butambi wa ng'wayo ubutu buzwalila shilungu
Kiswahili: Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
Do not leave your door open relying on a neighbor's good fortune.
Chubuka ikoba, utizuchubuka bongo
Kiswahili: Chubuka ngozi, usichubuke ubongo.
Peel the skin, do not peel the brain.
Kiswahili: Mpingo huzaa jivu.
Ebony wood bears ash.
Kiswahili: Mji wenye upinzani, haustawi.
A village full of conflict does not prosper.
Kiswahili: Aliyependa kumaliza kazi zote zake, alikufa bila kuoa.
The one who wanted to finish all their work died without marrying.
Kiswahili: Sikio halina maskini.
The ear has no poor person.
Kiswahili: Mikono ndiyo wazazi wa watu: fanya kazi kwa mikono yako uishi.
Hands are the parents of people: work with your hands and you will live.
Kiswahili: Meno meupe siyo moyo: kuchekacheka na kuonyesha meno si lazima kuwe ni dalili ya mtu mzuri.
White teeth are not the heart: smiling and showing teeth is not proof of a good person.
Kiswahili: Mkono mmoja hauchoti asali.
One hand cannot scoop honey.
Kiswahili: Tumbo halishukuru.
The stomach does not give thanks.
Kiswahili: Maskini hasa ni mtu aliyekufa.
The truly poor person is the one who has died.
Ng'wana nogu akalyaga nakabisile
Kiswahili: Mtoto mtii hula vizuri vingi, hata vilivyofichwa.
An obedient child eats well — even what was hidden.
Kiswahili: Mtenda mema huitwa mchawi (hulipwa maovu).
A doer of good is called a witch (and is repaid with evil).
Ngunda gwa kumhelo ishikilo shilili
Kiswahili: Shamba lililo pembeni hushambuliwa kila mara na wanyama na wadudu wabaya.
A field at the edge is always attacked by animals and pests.
Kiswahili: Aliyetumwa hauawi.
The messenger is not killed.
Njika magembe akibaga, wajika wakwe atibaga
Kiswahili: Mtu aliyezika majembe husahau, lakini aliyezika ndugu yake hasahau.
One who buries hoes forgets, but one who buries a relative never forgets.
Kiswahili: Mtu ni mkubwa akiwa anasimama.
A person is great when they stand firm.
Ntale ukunshiga ng'wigamu nomo utakashinga
Kiswahili: Mzee unaweza kumshinda mbio; humshindi kwa hekima.
You may outrun an elder, but you cannot outdo them in wisdom.
Uyo asusilve mbeho atitanilagwa moto
Kiswahili: Mtu akiwa na baridi, hangojei kuitwa asogee karibu kuota moto.
When someone is cold, they do not wait to be invited closer to the fire.
Kiswahili: Tembea uone.
Walk and see.
Yelelaga miso, utizuyelela lulimi
Kiswahili: Tembelea macho, usitembelee ulimi.
Visit with your eyes, not with your tongue.
Kiswahili: Nyuki huuma ovyo wakati wakiwa na asali.
Bees sting recklessly when they have honey.
Methali za Kisukuma (misemo) ni semi za jadi zinazofundisha hekima, kazi, umoja, malezi na maadili ya jamii ya Wasukuma. Kila msemo una maandishi ya Kisukuma pamoja na tafsiri ya Kiswahili na Kiingereza.
Kisukuma methali (misemo) are traditional Sukuma sayings that teach wisdom, hard work, unity, parenting, and community values. On Nukta Kamusi each entry has Kisukuma text plus Swahili and English meanings.
Kwa Kiswahili: "Mkono mmoja hauchoti asali." Inafundisha umuhimu wa kushirikiana — kazi kubwa haitendeki na mtu mmoja pekee.
Kisukuma is spoken mainly in Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita and nearby regions of northwestern Tanzania by the Sukuma people.
This page lists 26 Kisukuma methali (misemo) with Swahili and English meanings from community contributors.
Ukurasa huu una methali 26 za Kisukuma pamoja na maana za Kiswahili na Kiingereza.
The Kisukuma proverb "Ak'vambaga makono atabulagagwa" means: "Aombaye msamaha hauawi.". English: "One who asks for forgiveness is not killed.".
The Kisukuma proverb "Akalemela mbasa sumvua na nyabahanda" means: "Shoka limeshindwa kukata sembuse mundu?". English: "If the axe failed to cut, what about a blunt knife?".
The Kisukuma proverb "Buka mundi tukalye sha balimi" means: "Miguu yangu inukeni tukale vya wakulima, mvivu huishi kwa jasho la wenziwe.". English: "My feet, rise so we may eat the farmers' food — the lazy live off others' sweat.".
The Kisukuma proverb "Buli munda butisalamagwa" means: "Chakula kilichomo tumboni huwezi ukamgawia mwenzio hata kama anakufa.". English: "Food already in the stomach cannot be shared with a companion, even if they are dying.".
Chanzo: michango ya jamii ya Kisukuma. Unaweza kuchangia methali zaidi kupitia Unasemaje.